vidokezo vya sheria za Leba

Kujifunza na elimu ni safari. Ni mchakato unaoendelea wa muda mrefu. Elimu ndio inayowezesha uendelevu wa uchumi wa jamii na wa nchi kwa jumla.

Jifunze ‘kitu kimoja’ kila siku kutoka kwa chanzo cha kuaminika cha waalimu, watendaji na washauri katika sheria na uzoefu wa zaidi ya miaka 20. Mwaka huu, SheriaTips imeshirikiana na Haki Mashinani ili kuelimisha na kuwezesha waajiri na wafanyikazi na waajiri juu ya haki zao na majukumu mbali kama Sheria ya Kazi inavyotuelekeza. Kupitia teknolojia, Sheriatips iliunda jukwaa ambalo linaweza kutuma ujumbe mfupi, bila malipo, juu ya maswala yanayohusu haki za kazi, unyanyasaji wa kijinsia katika sehemu za ajira kati ya mada zingine. Mpokeaji baada ya kupokea ujumbe mfupi anaweza kuchagua kusoma yaliyomo zaidi ya ujumbe huo na hata kupata msaada wa kisheria kwa kutuma ujumbe wa pepe kupitia ukurasa huu ili kuelekezwa kwa NGO na wasaidizi wanasheria ambao wanasaidia bila malipo, na wanaojulikana kama ‘pro bono’ lawyers.

Angalia Maudhui mbali mbali kuhusu sheria za leba

 1. Haki ya mwajiri kukata ujira kwa kiasi kifaacho kisheria
 2. Haki ya mwajiri kukata ujira kwa siku ambazo kazi haijafanyika
 3. Haki ya waajiri kukata hela zifaazo kwa uharibifu wa mwajiriwa
 4. Mwajiri ana wajibu wa kukata kiwango cha hela zinzohitajika katika akiba za kimsingi za mwajiriwa.
 5. Wajiri wana haki ya kutoa taarifa kwa waajiriwa wao kuhusu sheria za kazini pamoja na adhabu yake.
 6. Jukumu la waairiwa kuwajibikia hela zilizo chini ya utunzi wao
 7. Haki ya kutarajia umakini na uangalifu pamoja na matumizi ya maarifa kutoka kwa waajiriwa.
 8. Haki ya kutarajia umakini na uangalifu pamoja na matumizi ya maarifa kutoka kwa waajiriwa.
 9. Uhuru wa Mwajiri kushiriki na shughuli za vikundi vya waajiri
 10. Mwajiriwa anafaa kutii maagizo ya kazini
 11. Mwajiriwa anafaa kufuata sheria kabla ya kujiuzulu kazini.
 12. Mwajiri lazima kufuata sheria anapomtimua mwajiriwa kazini.
 13. Wajibu wa mwajiriwa kutuma mavazi yafaayo kazini.
 14. Jukumu ya mwajiri kuhakikisha usalama na afya bora kazini.
 15. Haki ya mwajiri kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya mwajiriwa.
 16. Haki ya mwajiri kukagua utendakazi wa mwajiriwa.
 17. Haki ya mwajiriwa kulipwa mshahara wa mwezi mmoja anapoachishwa kazi.
 18. Haki ya mwajiri kumshusha mwajiriwa wake cheo kazini.
 19. Haki ya mwajiri kumpandisha mwajiriwa wake cheo.
 20. Haki ya mwajiri kuwataka waajiriwa kuwa waaminifu, waadilifu na wenye imani kwa mwajiri wao.
 21. Jukumu la mwajiriwa kutoingilia biashara ambayo ina ushindani na ile ya mwajiri wake.
 22. Wajibu wa mwajiri kuifadhi rekodi za waajiri wake.
 23. Haki ya mwajiri kushiriki uchaguzi katika vikundi vya waajiri
 24. Haki ya mwajiri kujuzwa mwajiriwa anapoondoka kwenda likizo
 25. Haki ya waajiriwa wa jinsia ya kike kwenda likizo ya uzazi
 26. Jukumu la kuwajuza waajiri kuhusu majeraha katika kazi
 27. Jukumu ya mwajiri kuhakikisha usalama na afya bora kazini.
 28. Haki ya mwajiri kutayarisha mkataba wa ajira
 29. Jukumu la waajiriwa kuifadhi siri za kazini.
 30. Mwajiriwa anafaa kufuata sheria kabla ya kujiuzulu kazini.

Wasiliana nasi!